Home » Predictions » Basketball
Katika ukurasa huu wa Gal Sport Betting, utakutana na habari bora za karibuni unazohitaji kwaajili ya mchakato kamili wa kubashiri mpira wa kikapu. Hii ni tovuti namba moja katika mtandao kwa kila shabiki na mpenzi wa mpira wa kikapu anayetafuta kuongeza maradufu faida yake ya kubashiri. Kwa usaidizi wa timu yetu ya wataalamu na wachambuzi waliobobea watakaokupa ushauri wa bure utaweza kugeuza ujuzi na ufahamu wako wa mpira wa kikapu utokanao na siku zote za kukesha bila kulala kuwa wa manufaa zaidi na kukuongezea kipato. Ubashiri wa mpira wa kikapu haujawahi kuwa rahisi kiasi hiki.
Mpira wa kikapu ni moja kati ya michezo maarufu zaidi katika historia ya michezo duniani. Ni mchezo unaochezwa katika kila nchi na kila bara duniani. Si kila mtu ni mzuri kwenye mpira kikapu na ndo sababu kubwa upo na timu yetu ya watalaamu na wachambuzi waliobobea watakaofanya mchakato wako mzima wa kubashiri mpira wa kikapu NBA kuwa wa kumbukumbu kubwa! Ni wazi hatuongelei tu kuhusu tu shirika la mpira wa kikapu Marekani NBA. Ubashiri wa mpira wa kikapu siku hizi unajumuisha mechi kutoka katika kila nyanja ya dunia na siku zote kuna timu bora inasubiri kujulikana kutoka katika ligi, nchi au bara moja au lingine.
Ukifuatilia tovuti yetu kwa karibu, wachambuzi wetu watakuhabarisha kuhusiana na habari muhimu unazotakiwa kufahamu ili kuweza kubashiri kwa makini. Tutakuhabarisha kuhusiana na ligi zote muhimu za mpira wa kikapu, mashindano ya kitaifa na kimataifa kutoka katika kila pande ya dunia. Fuatilia kwa makini kuweza kujua wachezaji bora ni wapi katika kila ligi husika ambao siku zote hurudisha faida maradufu kwa kubashiri kiwango cha point watakazozidisha katika kufunga. Kila mtu anaweza kufanya hivi! Na kama hafanyi basi ni kwanini asifanye kujiongezea kipato bila jasho?
Katika zama hizi za kubeti mitandaoni, mambo yanaenda kwa kasi sana na kwa faida kubwa mno kwa watumiaji yaani wabashiri. Kubashiri kwenye mpira wa kikapu nao kunazidi kukua kwa mfano sasa inawezekana kubashiria zaidi ya kitu kimoja au viwili ndani ya mechi moja ya kikapu. Unaweza kubashiria (kubetia) mchezaji mmoja kufunga zaidi au chini ya kiwango flani cha pointi, na unaweza ukafanya hivyo hivyo kwa upande wa timu pia bila kujalisha mshindi wa mechi itakuwa timu ipi. Unajali nini kuhusu mshindi wa mechi wakati mchezaji wako au timu yako imeshinda pointi zilizohitajika wewe kuwa mshindi kwa kubashiri?
Kujua tofauti kati ya timu dhaifu na timu nzuri kuna manufaa makubwa zaidi kwako.Kwanini ubashirie (ubetie) matokeo ya mwisho tu wakati unaweza kujishindia kiasi kikubwa kwa kubashiri timu itakofikia kiwango chake cha mwisho kwa muda flani cha madhambi (faulo) katikati ya mechi? Hiyo inatarajiwa kutoka kwako lakini sio kutoka kwa watu wengine, habari kama hii ni rahisi kutoifahamu au kuisahau lakini sio kama ukiwa na sisi na haswaa sio ukiwa na timu yetu ya wabashiri na wachambuzi waliobobea.
Kuna baadhi ya timu huanza mchezo kwa kasi na kulegeza kamba katikati ya mchezo lakini kupambana kufa na kupona katika dakika za mwisho za mechi. Saa nyingine ni bora zaidi kubashiri ni timu gani itashinda au kushindwa kipindi cha kwanza na cha tatu cha mchezo. Hii huitwa njia mbali mbali za kubashiri amabazo zitaongeza faida na ushindi wako maradufu.
Haijalishi kama unapendelea kubashiri katika ligi ya NBA au ligi nyingine yoyote ya kikapu, utapata ligi na zote na mashindano ya kikapu yote duniani. Ubashiri wa ligi ya NBA ya marekani upo juu sana kwenye orodha yetu na duniani lakini haimanishi kwamba sisi hatuna kitu kingine cha zaidi cha kukupa katika ulimwengu wa kubashiri mpira wa kikapu.
Bashiri kwa urahisi katika ligi zote za mpira wa kikapu ulaya kama vile ligi ya hispania ACB, Ligi ya urusi Super League 1, Adriatic ABA League, ligi ya ugiriki Greek A1 Ethniki na zingine kem kem kama vile ligi maarufu ya Brazili Brazilian Novo Basquete. Jukwaa letu la kuybashiri mpira wa kikapu haliishii kwenye ngazi ya vilabu tu. Katika tovuti ya Gal Sport Betting, utakuta makombe na mashindano ya kimataifa AfroBasket, EuroBasket, Olympics, FIBA Basketball World Cup. Kipengele hichi pia hakijasahau ligi za wanawake za mpira wa kikapu kama vile WNBA kwa starehe zako.
Jinsi maendeleo na dunia inavyokuwa kwa kasi watu wamekuwa wana muda mchache kila kukicha, hali ni hivyo hivyo katika ulimwengu wa kubashiri mpira wa kikapu. Watu wengi zaidi wamahamia katika kubashiri moja kwa moja mpira wa kikapu kwasababu inatokea kwa haraka sana ndani ya mechi moja, pia mkwanja wa kubashiri mpira wa kikapu nao unakuja kwa haraka zaidi, kuna muda mwingine unaweza umeingia tu kwenye ngwe ya pili ya kipindi cha mwisho (cha nne) na ukakuta timu inapambana ki sawa sawa kugeuza mchezo wanaokaribia kupoteza kuwa wa ushindi, amini usiamini kwamba ubashiri wa mpira wa kikapu NBA haujawahi kuwa wa kusisimua kiasi hichi kwa kukupa nafasi ya kujishindia maradufu kwa kubashiri wakati matukio yakiendelea mpaka filimbo ya mwisho wa mchezo.
Tunao watalaamu wenye ufahamu wa kutosha wa michakato ya kubashiri mpira wa kikapu watakaokupa ushauri, mbinu na vidokezo vya bure jinsi ya kujiongezea dau la ushindi wako. Watalaamu wetu pia watakupa tahadhari kama timu husika huwa haichezi vizuri inaposafiri nje ya uwanja wa nyumbani – au huwa ni moto wa kuotea mbali pale wanapocheza viwanja vya ugenini. Takwimu hizi hukusanywa, kuhesabiwa na kunyambuliwa na timu yetu ya watalaamu ili kukupa matokeo ya mwisho yenye faida – ushauri bora zaidi wa kubashiri mpira wa kikapu duniani.
Tunaelewa kwamba mara nyingi sababu ndogo tu inaweza ikabadilisha mwenendo mzima wa mchezo. Sababu hii ndo maana watalaamu wetu wa kuaminika hukabiliana na suala la kubashiri mpira wa kikapu kwa busara, utafiti na umakini mkubwa ili kutoa vidokezo na ushauri ulio bora zaidi – na uzuri wake haya yote ni BURE!
All correspondence to Director-General 27th Floor, PSSSF Twin Towers – Wing ‘A’,Mission Street. Gaming board of Tanzania license Number Sbl000000023 Issued on 14 Aug 2020. Fido Technologies LTD office Physical Address Livingstone Kariakoo, Block 63, Plot 7, Dar es Salaam, TANZANIA Gal Sport Betting is an adult site intended for players aged 18 or over, Winners know when to stop
© 2024 Fido Technologies LTD, All rights reserved®